• Contact us |
    • FAQ |
    • Comments |
    • Staff Mail |
TANZANIA EXTRACTIVE INDUSTRIES TRANSPARENCY INITIATIVE

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF MINERALS TANZANIA EXTRACTIVE INDUSTRIES TRANSPARENCY INITIATIVE

  • Home
  • About Us
    • History of TEITI
    • Organisation Structure
    • Working Group
    • Management Team
  • Partners
    • Government
    • Donors and Partners
    • Civil Socities
    • Extractive Companies
  • WorkPlan
  • TEITI Reports
    • Reports
    • Scoping Report
    • TEITI Annual Progress Report
    • Other Documents
    • Financial Statements
  • Opportunities
    • Tenders
    • Vacancies
    • TOR
  • Publications
    • Legislation
    • Policies
    • Contracts Disclosure
    • Minutes
    • EITI Standards
    • Speech
    • Licenses
  • Media Centers
    • Video Gallery
    • Photos Gallery
  • News
  • Infographics
    • Findings of 8th Report
    • Findings of 7th Report
    • Findings of 6th Report
    • Findings of 5th Report
  • Beneficial Ownership
  • Validations
  • Dashboard

Chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Uwazi katika usimamizi wa Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia waongezeka

Posted on: March 20th, 2025

CHINI YA UONGOZI WA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN UWAZI KATIKA USIMAMIZI WA SEKTA YA MADINI, MAFUTA NA GESI ASILIA WAONGEZEKA


•Akutana na Bi. Helen Clark mwenyekiti wa bodi ya EITI.

•Mkutano wa 62 wa bodi ya Kimataifa ya EITI wafanyika nchini.

•Ripoti za TEITI kutolewa kwa wakati.

•Tanzania ipo juu katika utekelezaji wa viwango vya Kimataia vya EITI. (Tathamini iliyopita ilionesha Tanzania ilipata 77/100).


 i)Uwekaji Wazi wa Ripoti za TEITI

Katika kipindi cha miaka minne (4), TEITI imefanikiwa kutoa ripoti nne (4) za TEITI kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019; 2019/2020; na 2020/2021; na 2021/2022. Ripoti hizo zimefanya ulinganishi wa malipo ya kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia na mapato kwa Serikali Kuu na katika Halmashauri ambazo zinapokea tozo (Service Levy) kwa mujibu wa Sheria ya Local Government Finance Act, 1982 . Ripoti hizo zinapatikana katika tovuti ya TEITI (www.teiti.go.tz).



 ii)Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Dkt. Samia Suluhu Hassan, alihutubia Mkutano wa Kimataifa ya EITI

Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alihutubia Mkutano Mkuu wa Asasi ya Kimataifa ya EITI (EITI Global Conference) uliofanyika Dakar- Senegal. Ushiriki wa Mkutano huu kama nchi ni ishara ya uimara wa nchi katika utekelezaji wa vigezo vya kimataifa vya uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa  rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia. Mkutano huu ulihudhuliwa na washirki zaidi ya 1,500 kutoka nchi wanachama ya Umoja wa Kimataifa Duniani.



 iii)Kupitishwa kwa Muundo wa TEITI (Organization Structure)

Katika kipindi cha miaka minne (4) ya uongozi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu, Muundo na mgawanyo wa majukumu ya Taasisi ya TEITI ulipitishwa. Kuidhinishwa kwa Muundo huo kutawezesha utekelezaji wa majukumu ya Taasisi kikamilifu na kwa ufanisi.


 iv)Utekelezaji wa Sheria ya TEITA, 2015

Katika utekelezaji wa Sheria ya TEITA, 2015, TEITI imeongeza uwazi juu ya matumizi ya mapato ya Halmashauri yanayotokana na tozo ya huduma (Service Levy) na malipo yanayohusu wajibu wa makampuni kwa jamii (Corporate Social Responsibility (CSR)) kutoka kampuni za uchimbaji wa Madini, Mafuta na Gesi Asilia. Aidha TEITI ipo katika hatua za mwisho katika takwa la Sheria ya TEITA, 2015 la uwekaji wazi wa Mikataba ambao Serikali imeingia na kampuni za Madini, Mafuta na Ges Aslia.



 v)Uteuzi wa Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan - Rais wa Jamuhuri ya muungano alimteua CPA. Ludovick Utouh kuwa Mwenyekiti wa kamati ya TEITI kusimamia shughuli za kamati ya TEITI chini ya kifungu cha tano (5) cha Sheria ya TEITA, 2015 ya utekelezaji wa shughuli za kuhamasisha uwazi na uwajibikaji katika sekta Madini,Mafuta na Gesi Asilia.



 vi)Ushiriki wa TEITI katika Uhamasisha matumizi ya takwimu zinazotolewa na ripoti za TEITI

TEITI ilishiriki na kutoa elimu kuhusu majukumu yake wakati wa Maonesho mbalimbali yakiwemo maonesho ya kimataifa ya sabasaba, nanenane na maonesho ya kitaifa ya uwekezaji katika sekta ya madini Mkoani Geita. Aidha, TEITI imeshiriki katika warsha mbalimbali kuelimisha umma juu ya matumizi takwimu zinazotolewa na ripoti za TEITI za kila mwaka katika kuhoji juu ya manufaa ya rasilimali hizo kwa wananchi na nchi kwa ujumla.  TEITI imefanya warsha Mikoa ya Geita, Mwanza, Songwe, Mtwara na Lindi. Aidha kundi maalum la wananchi wasioona walihusishwa katika uhamasishaji huo.


 vii)Kuratibu Mkutano wa Bodi ya Kimataifa EITI

TEITI imeratibu kufanyika kwa Mkutano wa 62 wa Bodi ya Kimataifa ya EITI uliofanyika hapa nchini tarehe 13 na 14 Machi, 2025. Mkutano huo wa Bodi ni fursa kwa nchi na Watanzania kwa ujumla kwa kuwa Tanzania ilipokea ugeni wa zaidi ya washiriki mia moja ikijumuisha wawakilishi wa Makapuni Makubwa duniani yanayojihusisha na Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia hivyo ni Kivutio cha Uwekezaji katika nchi yetu, Vilevile, ni fursa ya kuongeza fedha za kigeni kwa kuwa wageni hao walitumia bidhaa na huduma hapa nchini.



 viii)Ujio wa Rt. Hon. Helen Clark – Mwenyekiti wa bodi ya kimataifa ya EITI

Katika kuimarisha ushirikiano kati ya Taasisi ya Umoja wa Kimataifa ya Uwazi na Uwajibikaji na nchi ya Tanzania, mwenyekiti ya Bodi wa EITI, Rt. Hon. Helen Clark aliyetembelea Tanzania na kufanya mazungumzo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mawaziri wa Nishati na Madini hapa nchini lengo likiwa ni kujadili utekelezaji wa shughuli za uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali Madini Mafuta na Gesi Asilia.


ix) TEITI imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Asasi za Kiraia, Serikali na Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia katika utekelezaji wa masuala ya uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia kulingana na Sheria ya TEITA, 2015.



 x)Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za EITI hapa nchini

TEITI ilifanyiwa Tathmini (validation) ya utekelezaji wa shughuli za uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia na Bodi ya Asasi ya Kimataifa ya EITI. Matokeo ya tathmini hiyo yanaonesha kuwa Tanzania imepata daraja la moderate (Daraja la tatu) katika kutekeleza vigezo vya EITI vya mwaka 2019 ambapo Tanzania imepata alama  77/100 kwa kuzingatia maeneo matatu ambayo ni Stakeholder engagement (82.5), Transparency(73.5) pamoja na Outcome and impact (75.5). Bodi hiyo imepongeza juhudi za Serikali na wadau mbalimbali katika kufanikisha utekelezaji wa shughuli za EITI hapa nchini.

Announcements

  • Uteuzi wa Wajumbe wa Taasisi - TEITI March 01, 2023
  • President's Office Public Service Recruitment Secretariat Vacancy Announcement April 03, 2023
  • Request For Expression of Interest August 17, 2018
  • VACANCIES ANNOUNCEMENT May 02, 2018
  • View All

Latest News

  • Rais Mwinyi Afungua Rasmi Maonesho ya Sabasaba 2025

    July 07, 2025
  • STAMICO na TEITI Waahidi Kuendeleza Ushirikiano katika Utekelezaji wa Viwango vya Kimataifa vya EITI

    July 07, 2025
  • Mgeni Rasmi Katika Ufunguzi wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba - Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

    July 07, 2025
  • Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba - 2025 Fahari ya Tanzania

    July 07, 2025
  • View All

Video

Mhe. Rais Dkt Samia Akishiriki Maadhimisho Ya Siku Ya Mashujaa, Mtumba-Dodoma.
More Videos

Quick Links

  • Events
  • EITI
  • TEITI yawaongezea maarifa wananchi kuhusu rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asili
  • Tenders
  • Announcements
  • History of TEITI

Related Links

  • Ministry of Minerals
  • The Ministry of Energy
  • The Mining Commisssion
  • Petroleum Upstream Regulatory Authority(PURA)
  • Tanzania Petroleum Development Corporation(TPDC)
  • The Ministry of Finance
  • EITI Secretariate
  • Geographical Survey of Tanzania

Visitors Counter

https://www.Stat-Counter.org

World visitors tracker

world map hits counter

Location Map

TANZANIA EXTRACTIVE INDUSTRIES TRANSPARENCY INITIATIVE

Contact us

    TEITI Office Dodoma

    Postal Address: Government City, Mtumba, S.L.P 361 Dodoma, Tanzania Email: info@teiti.go.tz

    Telephone: +255688386546

    Mobile: +255688386546

    Email: info@teiti.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.