• Contact us |
    • FAQ |
    • Comments |
    • Staff Mail |
TANZANIA EXTRACTIVE INDUSTRIES TRANSPARENCY INITIATIVE

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF MINERALS TANZANIA EXTRACTIVE INDUSTRIES TRANSPARENCY INITIATIVE

  • Home
  • About Us
    • History of TEITI
    • Organisation Structure
    • Working Group
    • Management Team
  • Partners
    • Government
    • Donors and Partners
    • Civil Socities
    • Extractive Companies
  • WorkPlan
  • TEITI Reports
    • Reports
    • Scoping Report
    • TEITI Annual Progress Report
    • Other Documents
    • Financial Statements
  • Opportunities
    • Tenders
    • Vacancies
    • TOR
  • Publications
    • Legislation
    • Policies
    • Contracts Disclosure
    • Minutes
    • EITI Standards
    • Speech
    • Licenses
  • Media Centers
    • Video Gallery
    • Photos Gallery
  • News
  • Infographics
    • Findings of 8th Report
    • Findings of 7th Report
    • Findings of 6th Report
    • Findings of 5th Report
  • Beneficial Ownership
  • Validations
  • Dashboard

TEITI Kuzindua Ripoti ya 15 ya Uziduaji

Posted on: February 20th, 2025

TEITI KUZINDUA RIPOTI YA 15 YA UZIDUAJI


Yatoa elimu kwa watu wenye uono hafifu


TAASISI ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) imepanga kuweka wazi ripoti ya 15 ya TEITI kabla ya Juni mwaka huu.


Hayo yameelezwa leo Februari 20, 2025 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI, Ludovick Utouh kupitia hotuba iliyosomwa na Kaimu Meneja Kitengo cha Uwazi na Uwajibikaji ya TEITI, Erick Ketagory wakati wa kuzindua semina maalumu ya kuhamasisha matumizi ya takwimu za ripoti za TEITI kwa wanachama wa Chama cha Wasioona waliotoka wilaya zote za Mkoa wa Dodoma, Chimwino, Bahi,Dodoma mji, Kongwa,

Kondoa, Mpwapwa, Udom, Shule ya Msingi Buigiri, Shule Msingi Homboro Bwawani, Kamati ya Utendaji Mkoa wa Dodoma, Chemba,

Kamati Mkoa.


Alisema mpaka sasa TEITI imesatoa ripoti 14 na kwa sasa ipo katika maandalizi ya ripoti ya 15 kwa kipindi cha Julai 1, 2022 hadi Juni 30, 2023 na itawekwa wazi kabla ya Juni mwaka huu.


TEITI hutakiwa kuweka wazi malipo ya kodi na mapato yaliyofanywa na kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia kwa Serikali kila mwaka.


Hadi sasa Tanzania imechapisha na kutoa ripoti 14 kwa kipindi cha Julai 1, 2008 hadi Juni 30, 2022 zinazolinganisha malipo yaliyofanywa na kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asili na mapato yaliyopokelewa na Serikali.


Ripoti ya 14 ya TEITI ambayo hutolewa katika kutimiza matakwa ya Kimataifa ya Uwazi na Uwajibikaji (EITI) ilionesha kuwa sekta ya madini ilichangia asilimia 80.21 ya Mapato yote ya Serikali yatokanayo na rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia kwa mwaka 2021/22.


Aidha, Ketagory alisema pia TEITI imekuwa ikiandaa na kuchapisha kwa waandishi maalum ya nukta nundu ili kuwafikia kundi la wananchi wasioona hapa nchini, mtakumbuka kuwa rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asili ni za wananchi wote.


“Hivyo TEITI imeona ni vyema kuandaa ripoti zetu kwa nukta nundu ili wananchi wote wapate fursa ya kuelewa na kufahamu juu ya taarifa na takwimu mbalimbali katika sekta Madini, Mafuta na Gesi Asilia ili waweze kuhoji manufaa ya rasilimali hizo kwa nchi na wananchi.”


Akisoma hotuba ya Katibu Mtendaji wa TEITI, Mariam Mgaya, Kaimu mkuu wa kitengo cha Tehama na Takwimu TEITI, Bakari Birika katika warsha hiyo washiriki watapata fursa ya kupata uelewa kuhusu majukumu ya TEITI na namna ya kutumia takwimunzinazoandaliwa kupitia Ripoti za TEITI.


“Taasisi inajukumu la kujenga mfumo wa uaandaji wa Ripoti za TEITI na kuwajengea uwezo wananchi katika kutumia Takwimu zinazotokana na taarifa za TEITI kupitia warsha mbalimbali na ndio maana tumeandaa warsha hii kwa kundi hili ili nao wawe na mchango wa kuchangia katika sekta hizi.”


Aidha, Birika alisema mpango wa TEITI pia imepanga kuweka wazi mikataba ambayo serikali imeingia na kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia na kujenga rejista ya wamiliki wa kampuni za madini, mafuta na gesi asilia.


Naye Mwenyekiti Chama cha Wasioona Mkoa wa Dodoma, Omari Lubuva alishukuru kwa mafunzo hayo ambayo yatawasaidia wao kupata uelewa kuhusu TEITI na kujua fursa zilizopo.


“Makundi ya walemavu hususani wasio ona wamekuwa wakisahaulika katika mambo mengi, hivyo tunaishukuru TEITI kwa kuona umuhimu wa sisi kupata elimu na uelewea na kutambua fursa zilizopo na kuzitumian kama ilivyo kwa watanzania wengine.”

Announcements

  • Uteuzi wa Wajumbe wa Taasisi - TEITI March 01, 2023
  • President's Office Public Service Recruitment Secretariat Vacancy Announcement April 03, 2023
  • Request For Expression of Interest August 17, 2018
  • VACANCIES ANNOUNCEMENT May 02, 2018
  • View All

Latest News

  • Watumishi wa TEITI Washiriki Kikamilifu Mei Mosi, 2026 Jijini Dodoma

    May 01, 2026
  • Sekta ya Madini Yang'ara Uwekezaji, Bei ya Dhahabu Yaendelea Kupanda

    April 27, 2026
  • Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI wafanya ziara Mgodi wa Dhahabu wa Geita

    March 11, 2026
  • Senyamule awataka Wanawake Kuongeza Bidii kwenye Uthubutu

    March 08, 2026
  • View All

Video

Hotuba ya Wizara ya Madini Kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027
More Videos

Quick Links

  • Events
  • EITI
  • TEITI yawaongezea maarifa wananchi kuhusu rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asili
  • Hotuba ya Wizara ya Madini 2026-2027
  • Tenders
  • Announcements
  • History of TEITI

Related Links

  • Ministry of Minerals
  • The Ministry of Energy
  • The Mining Commisssion
  • Petroleum Upstream Regulatory Authority(PURA)
  • Tanzania Petroleum Development Corporation(TPDC)
  • The Ministry of Finance
  • EITI Secretariate
  • Geographical Survey of Tanzania

Visitors Counter

https://www.Stat-Counter.org

World visitors tracker

world map hits counter

Location Map

TANZANIA EXTRACTIVE INDUSTRIES TRANSPARENCY INITIATIVE

Contact us

    TEITI Office Dodoma

    Postal Address: Government City, Mtumba, S.L.P 361 Dodoma, Tanzania Email: info@teiti.go.tz

    Telephone: +255 26 2610760

    Mobile:

    Email: info@teiti.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2016 TEITI . All rights reserved.